FM Manyara
FM Manyara
19 June 2026, 12:52 am

Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara imezindua kampeni ya siku 14 ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu malezi chanya chini ya kauli mbiu inayosema ”mtoto ni malezi Msingi wa familia bora kwa taifa imara”.
Uzinduzi huo umefanyika june 18 mwaka huu 2026 katika kiwanja cha shule ya sekondari mamire nakuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo shirika la So They Can Tanzania (STC) na Amani Girls.
Ujumbe wa risala ya wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari mamire siku ya Mtoto wa Africa ambapo maadhimisho yake yatafanyika june 30 umeelezea changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwaathiri watoto nakudumaza maendeleo yao kitaaluma na kiafya ikiwemo ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo ambaye ni diwani wa kata ya Mamire Augustino Sosiya ameitaka jamii kupokea ujumbe huo kwa siku zote hizo huku akisema kauli mbiu ya mwaka huu ndio dhima ya msingi wakufanikisha adhma hiyo.
Akitoa salamu kwa niaba ya Shirika la So They Can Tanzania (STC) Mzazi mahiri kutoka kata ya Mamire Issa Nkunga amesema wazazi na jamii inapaswa kushirikiana na kuendelea kumlinda mtoto dhidi ya ukatili na kuhakikisha anapatiwa elimu itakayomsaidia kufikia malengo yake.
Sherehe hizo za uzinduzi wa siku 14 zimepambwa na burudani mbali mbali ikiwemo nyimbo, Mashairi mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo kata ya Mamire, Galapo, Qash na Endakiso.
