FM Manyara

Elimu ya nishati safi ya kupikia yafika NMB Babati

5 August 2026, 10:05 pm

Picha ya maafisa uhusiano TANESCO wakitoa elimu ya Nishati safi ya kupikia

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Babati mkoani Manyara wamepata elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya umeme ya kupikia, huku wakihimizwa kutumia teknolojia hiyo kwa manufaa ya afya, mazingira na uchumi.

Na Mzidalfa Zaid

Elimu hiyo, iliyotolewa na maafisa wa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Manyara, iliambatana na maonesho ya kupika kwa vitendo yaliyolenga kuongeza uelewa kuhusu faida za kutumia majiko ya umeme, ikiwemo kuokoa muda na gharama, kulinda afya ya mtumiaji pamoja na kuhifadhi mazingira.

Baada ya mafunzo hayo, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NMB, Thomas Ninga, aliishukuru TANESCO kwa kutoa elimu hiyo akisema imewasaidia kuelewa kwa kina manufaa ya kupikia kwa umeme.

Elimu hiyo ni sehemu ya kampeni ya TANESCO ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi na taasisi mbalimbali nchini.