FM Manyara
FM Manyara
15 September 2026, 1:55 pm

Kambi ya Matibabu ya afya inayoratibiwa na Shirika la So They Can Tanzania (STC) imeanza rasmi sept 14 katika shule ya msingi OIM iliyopo kata ya Galapo Wilayani Babati mkoani Manyara ambayo itafanyika kwa siku sita.
Na Marino Kawishe
Akizungumzia huduma zitakazotolewa kwenye kambi hiyo Meneja wa shirika la STC Tanzania Roselyne Mariki amesema huduma zitolewazo ni pamoja na uchunguzi wa Saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, Huduma za uchunguzi wa macho pamoja na vipimo vingine ikiwemo kinywa na Meno na uchunguzi wa afya ya akili na ushauri na sahaa.
Naye Mratibu wa kambi hiyo ya Afya na Muuguzi mkuu kutoka Hospital ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Sister Thea Funto amewataka wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Halmashauri hiyo hasa kwenye kata zitakazofikiwa na kambi hiyo kujitokeza kwa wingi kupata matibabu ambayo yanaratibiwa Bure na Shirika hilo.
Kambi hiyo ya afya iliyoanza sept 14 imefadhiliwa na shirika la So They Can Tanzania, KCCO, Kafika House, FreeO2, Sibusiso na Chuo cha ualimu maalumu Patandi na itaendelea tena kwa siku tano katika kata za Galapo, Qash, Endakiso na Mamire zilizopo Wilayani Babati mkoani Manyara.

Mwananchi akipatiwa huduma ya Vipimo vya Macho katika kambi ya matibabu Gallapo