FM Manyara

RC Sendiga azindua tisheti za Manyara Tanzanite Marathon

17 August 2026, 12:47 pm

Picha ya mkuu wa mkoa waManyara Queen Seniga

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, leo amezindua tisheti rasmi zitakazotumika katika mbio za hisani za Manyara Tanzanite Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Agosti 22 mwaka huu.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sendiga amesema hadi kufikia asubuhi ya leo, jumla ya watu 2,200 wamekwishajisajili kushiriki katika mbio hizo za hisani, huku wananchi 123 wakijisajili kushiriki katika utalii wa ndani kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Andrew Method, amesema mwitikio wa wananchi katika kushiriki mbio hizo umekuwa mkubwa, huku akiwataka wananchi ambao bado hawajajisajili kutumia fursa hiyo kujiandikisha, na wale ambao tayari wamejisajili kuendelea kuchukua tisheti zao za mbio hizo.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Andrew Method,

Nao baadhi ya washiriki waliopokea tisheti hizo wamesema wameshiriki katika mbio hizo kwa lengo la kuimarisha afya zao, pamoja na kuchangia katika kuokoa maisha ya watoto wachanga, hususan watoto njiti.

Sauti ya washiriki

Manyara Tanzanite Marathon inatarajiwa kufanyika Agosti 22 mwaka huu, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. Mbio hizo zinafanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto.”

picha ya baadhi washiriki wakiwa wamevaa jezi