FM Manyara

TANESCO Manyara yaonya wananchi uharibifu wa miundombinu

12 May 2026, 5:43 pm

picha ya baadhi ya miundombinu ya TANESCO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Manyara limetoa tahadhari kwa wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya kuhujumu miundombinu ya umeme, ikiwemo kuiba mafuta ya transfoma na kusababisha kukatika kwa umeme pamoja na kuchoma nguzo. 

Na Emmy Peter

Akizungumza na Manyara FM, Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Samueli Mandari, amesema kuwa kila mwananchi anatakiwa kulinda miundombinu ya umeme katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale anapobaini vitendo vya uharibifu au hujuma dhidi ya miundombinu hiyo, ili hatua za kisheria zichukuliwe mapema.

Aidha, Mandari amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na miundombinu ya umeme kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa, badala ya kuendelea kuharibu miundombinu hiyo, kwani vitendo hivyo vinaathiri maendeleo ya jamii na uchumi kwa ujumla.