FM Manyara

  RC Sendiga azindua  gari la milioni 180 Simanjiro

24 June 2026, 1:16 am

Picha ya Bus Jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara

  

Mkuu wa mkoa wa Manyara,Queen Sendigaamezindua gari la halmashauri  ya wilaya ya Simanjro  lenye thamani ya shilingi milioni 180, litakalotumika kwenye shughuli mbalimbali za kuwahudumia wananchi wa wilaya hiyo.

Sendiga amezindua gari hilo  leo alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi mbali mbali itakayotembelewa na kugaguliwa na mwenge wa uhuru kwa mwaka 2026 akisema gari hilo litasaidia shughuli zinazofanywa na watumishi wa wilaya hiyo ya simanjiro pamoja na kuwahudumia wananchi.

Aidha, Sendigaameipongeza  halmashauri ya wilaya Simanjiro kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara (wa katikati) pamoja na mkuu wa Wilaya ya Simanjiro