FM Manyara
FM Manyara
8 August 2025, 2:03 pm

Baada ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) kutangaza bei mpya ya mafuta ambayo imeanza kutumika mwezi Agast , kwa kanda ya kaskazini wafanyabiashara wa mafuta wametakiwa kuuza mafuta kwa bei elekezi.
Na Mzidalfa Zaid
Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini Lorivii Long’idu, amesema hayo wakati akiongea na fm Manyara, amesema bei mpya imeanza kutumika jumatano ya wiki hii na kusema kuwa bei ya mafuta imeshuka ukilinganisha na bei ya mafuta kwa mwezi uliopita.
Katika hatua nyigine amesema EWURA imeshiriki maonesho ya wakulima nane nane ambayo yanaendelea katika viwanja vya njiro jijini arusha na wametoa elimu kwa wananchi kuhusu maji,gesi na nishati.
Kwa upande wake afisa huduma kwa wateja kutoka EWURA Kanda ya kaskazini Bahati Bakunda amewataka wananchi kutembelea banda la EWURA linalopatikana katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha ili kupata elimu juu ya kazi kubwa inayofanywa na EWURA.