FM Manyara

Zaidi ya wananchi  5,000 Endamaghay  wanufaika na mradi wa maji 

14 July 2026, 11:38 pm

Picha ya Kiongozi wa Mabio za  Mwenge wa uhuru kitaifa Wazo Michael Mwang’onda akifungulia bomba la maji pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remideus Mwema akiwa anakinga ndoo ya maji katika mradi wa maji wa Endamaghay .

Zaidi ya wananchi 5,000 kutoka vijiji vitatu 3 vilivyopo wilayani Babati mkoani Manyara, wamenufaika  na mradi wa maji  wa Endamaghay uliolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama uliogharimu shilingi Bilion 1.9

Na Emmy Peter

Mradi huo umezinduliwa na Kiongozi wa Mabio za  Mwenge wa uhuru kitaifa Wazo Michael Mwang’onda ambapo  amesema utekelezaji wa mradi huo  unaunga mkono juhudi za serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassani za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji na kupunguza adha ya kubeba maji kichwani, hususan kwa wanawake na watoto.

Sauti ya Kiongozi wa Mabio za  Mwenge wa uhuru kitaifa

Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara, James Kionaomela, amesema mradi huo unahusisha tanki la kuhifadhi maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 na utawawezesha wananchi kuunganishiwa huduma ya maji moja kwa moja majumbani, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa maji kwa jamii.

Sauti ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara

Aidha,baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo wameishukuru Serikali  ya awamu ya sita kwa utekelezaji wake, nakusema  mradi huo wa maji utawasaidia kuepuka kutembea umbali  mrefu  kufuata  huduma ya maji  pamoja na kuongeza fursa za kufanya shughuli za maendeleo .

Sauti za wananch wa Endamaghay