FM Manyara

Mwenge wa uhuru waweka jiwe la msingi katika daraja la Sigino – Komoto

15 July 2026, 10:56 pm

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Wazo Michael Mwang’onda akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja la Sigino -Komoto Mkoani Manyara

Mwenge wa uhuru umekagua na kuweka jiwe la msingi katika daraja la Sigino – Komoto linalounganisha kata ya sigino na kata ya Komoto halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara

Na Benny Akaro

Mradi huo unaotekelezwa chini ya wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA Umegharimu kiasi cha shilingi milioni 900.4

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Wazo Michael Mwang’onda amesema mwenge wa uhuru umefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo akiwataka wananchi kuulinda na kuutunza ili uweze kuleta kudumu

Amesema  Serikali inaendelea kuboresha na kuwekeza katika miundombinu ya barabara kwa lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi na kimaendeleo.

Sauti ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa Tarura wilaya ya Babati, Eng. Aloyce Nombo amesema mradi huo ulikadiriwa kukamilika  Mei 2026 lakini kutokana na changamoto za hali ya hewa kwasasa unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwezi agosti mwaka huu.

Sauti ya Meneja wa Tarura wilaya ya Babati

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mh. Emanuel Khambay ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo ambao uko mbioni kukamilika.

Naye, Naibu waziri wa OR-Utumishi & Utawala Bora Bi.Regina Ndege amesema daraja hilo ni fursa kiuchumi wa wananchi wa pande zote mbili kwa kuwa linaenda kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kupata huduma na kuuza na kununua  bidhaa.

Mradi huo ni miongoni mwa miradi  saba yenye thamani ya shilingi Bilioni 8.09 iliyopitiwa na mwenfe wa uhuru 2026 katika halmashauri ya mji wa Babati.

Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2026 *Amani, Umoja na Mshikamano wa Kitaifa*