FM Manyara
FM Manyara
14 May 2026, 5:22 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ametoa maagizo kwa wataalam wa mipango miji mkoani Manyara kuhakikisha wanafatilia eneo la ujenzi kwa wananchi kabla hawajatoa kibali cha ujenzi.
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga amesema hayo katika kikao cha Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati baada ya kubaini uwepo wa ujenzi holela katika eneo la daraja la Mrara kwa kukiuka taratibu za mazingira kutokana na kutofika mita60 kutoka eneo la mto .
Aidha, amesema mji wa Babati unakua kwa kasi kiuchumi,na majengo yanapaswa yajengwe kwa utaratibu, ambapo amewaonya maafisa mipango mji wanaotoa vibali hivyo bila kufika eneo husika.