FM Manyara
FM Manyara
16 April 2026, 8:17 pm

Wanafunzi 104 wa kidato Cha sita wa shule ya sekondari ya wasichana Manyara, wamehitimu Leo ambapo wanafunzi hao wameishukuru serikali kwa kufanikisha kufika hatua hiyo.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara,mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala, amesema shule hii Hadi kukamilika imetumia shilingi bilioni 4.5 na hii ni kutokana na juhudi za serikali za kukuza elimu.
Amewasihi wahitimu hao kuendelea kusoma kwa bidii pamoja na kuepuka kufanya matendo maovu ikiwemo uvutaji wa dawa za kulevya, pombe au michezo ya kubahatisha .

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya wasichana ya Manyara Gisela Msoffe,amesema shule hiyo Ina jumla ya wanafunzi 510 na imekuwa kifanya vizuri katika mtihani mbalimbali kwa Kanda ya kaskazini.

Nao baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu katika shule hiyo,wamesema elimu ambayo wameipata wataendelea kuifanyia kazi huko waendako.
Aidha, mgeni rasmi katika mahafali hayo ambae ni mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo kujenga uzio, kuongeza Matank ya maji n.k
