FM Manyara

Tundu Lisu kuunguruma Manyara

April 25, 2024, 9:25 pm

Picha ya makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.

Chadema kufanya maandamano ya amani mkoani Manyara Tarehe 26/04/2024 ,kwa  lengo la kuishinikiza Serekali kupunguza ukali wa maisha kwa watanzania pamoja na kuwapatia katiba mpya,

Na George Agustino

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kesho kinatarajia kufanya maandamano ya amani katika mkoa wa Manyara ambayo yatafanyika katika mji wa Babati na kuongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu .

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini babati mkoani hapa katibu wa chadema kanda ya kaskazini Amani Golugwa  amesema maandamano hayo ni ya amani kwa  lengo la kuishinikiza serikali kupunguza ukali wa maisha kwa watanzania pamoja na kuwapatia katiba mpya,

Sauti ya  katibu wa chadema kanda ya kaskazini Amani Golugwa