FM Manyara
FM Manyara
30 April 2026, 1:34 pm

Wananchi wametakiwa wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kuzingati mlo kamili kwa kula vyakula vyenye lishe na sio kula kwa mazoea huku waisisitizwa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuweka Afya zao vizuri.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda kwenye kikao cha Tahimini ya Lishe kwa kipindi cha robo ya Tatu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, na kusema watu wengi wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo uzito uliopitiliza kutokana na kukosa lishe bora.
Kwa upande wake Mratibu wa Lishe ambaye ni Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Babati Erick Bunziya amesema kwa robo ya nne wataendelea na kuhamasisha wananchi kulima na kutumia mazao ya asili yaliyoko katika maeneo yao katika kutengeneza chakula chenye virutubisho sahihi.
Nae mganga mkuu wa halimashauri ya wilaya ya Babati dokta Madama Hosea, amesema wananchi bado wanahitaji elimu ya lishe ili i wasiwe na mazoea ya kula ulaji usiofaa ili watoto wasipate changamoto ya utapiamlo au ukubwa uliopitiliza kwa watu wazima.
