FM Manyara

Tanesco  Manyara, yaendeleza  matumizi ya nishati safi ya kupikia

22 April 2026, 5:47 pm

Picha ya Afisa uhusiano Tanesco mkoa wa  wa Manyara Samuel Mandari

Wiki ya nishati ikiwa naendelea  kuadhimishwa katika maeneo mbalimbai nchini, shirika la umemee tanzania tanesco mkoa wa manyara limeindelea na ugawaji wa majiko ya nishati safi ya umeme katika maeneo mbali mbali ya mji wa babati.

Na Emmy Peter

Afisa uhusiano Tanesco mkoa wa  wa Manyara Samuel Mandari amesema zoezi hilo linaendelea mkoani Manyara  ambapo ni juhudi za kuunga mkono serikali katika matumizi ya nishati safi  ya kupikia kwa wananchi.

Aidha amesema  majiko hayo yanafaida kwa watumiaji na inaokoa garama kwa mwananchi ambapo  amesema  malipo hayo ni nafuu na utalipa kupitia mita ya umeme unayo tumia.

saut ya Afisa uhusiano Tanesco mkoa wa  wa Manyara Samuel Mandari

Sambamba na hayo  amesema lengo la ugawaji wa majiko hayo yanayotumia umeme ni kuwasaidia wananchi kupika kwa urahisi na haraka ambapo amewataka mama lishe kutumia nishati hiyo katika biasharaa zao .

Kauli mbiu ya nishati safi katika mkoa wa Manyara ni pika kijanjaa pika na umemee .