FM Manyara
FM Manyara
2 July 2026, 12:54 am

Na Emmy Peter
Mkurugenzi wahalmashauri ya Mji wa Babati CPA Shabani A. Mpendu amesema Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2026 unatarajiwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.07.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake amesema maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanaendelea vizuri,na halmashauri ikihakikisha miradi yote iliyopangwa kufikiwa na mwenge wa uhuru inakamilika kwa wakati na kuonesha mafanikio ya utekelezaji wake kwa wananchi.
Aidha Mpendu amesema lengo la Mwenge wa Uhuru ni kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na usimamizi mzuri wa miradi inayowanufaisha wananchi, sambamba na kuhimiza uzalendo, mshikamano na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake Mratibu wa mbio za Mwenge mkoa wa Manyara Samweli Pastor amesema Halmashauri za wilaya Mkoani Manyara zinatakiwa kuendelea kuratibu kikamilifu wiki ya vijana kabla ya kuanza mbio za Mwenge wa uhuru ambao utakimbizwa wilaya zote za mkoa wa Manyara kuanzia julai 12 mwaka huu.