FM Manyara

Babati TC yaibuka mshindi bonanza la miaka 62 ya muungano

26 April 2026, 11:10 am

Picha ya baadhi ya watumishi wa halmashauri ya mji wa Babati wakisherehekea ushindi

 Babati TC yang’ara na kuibuka mshindi wa jumla katika Bonanza la Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika Jana kwa ngazi ya Mkoa wa Manyara katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.

Na Mzidalfa Zaid

Halmashauri ya Mji wa Babati imeibuka mshindi wa jumla katika bonanza hilo la Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Michezo iliyochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu, mbio za kwenye magunia na riadha.

Aidha, Halmashauri ya Mji wa Babati imeweza kuongoza katika michezo ya mpira wa miguu na mpira wa pete kwa kuzishinda timu zote za Mkoa wa Manyara.

Picha ya baadhi ha washiriki wa michezo