FM Manyara
FM Manyara
16 July 2026, 6:57 pm

Mkoa wa wa Manyara unatarajia kuja na mkakati wakutomeza ukeketaji Tanzania ambao utafika kwenye halmashauri ya wilaya ya Mbulu iliyoshamiri zaidi kwa vitendo hivyo.
Na Marino Kawishe
Serikali mkoani Manyara imesema inaendelea kupambana na vitendo vya ukatili vilivyoshamiri kwenye baadhi ya maeneo mkoani hapa na wakija na mkakati wakutomeza ukeketaji Tanzania ambao utafika kwenye halmashauri ya wilaya ya Mbulu iliyoshamiri zaidi kwa vitendo hivyo.
Akizungumza na fm Manyara Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Manyara Anna Fiso amesema lengo la mpango huo kwa mkoa nikuhakikisha elimu ya ukatili inafika kwenye jamii na kupunguza kwa kiwango kikubwa ukatili ambao ni asilimia 43 kwasasa.
Aidha afisa ustawi wa jamii mkoa wa Manyara Khadija Muango amesema mpango huo unaanza na wilaya ya mbulu na baadae halmashauri nyingine nakusema mpango huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano 2026-2030.