FM Manyara

Waumini wahamasishwa kuchangia ujenzi msikiti mkuu Manyara

24 May 2026, 9:31 pm

Picha ya Shekhe Mkuu wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi

Waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na jamii kwa ujumla mkoani Manyara wametakiwa kuwa na umoja na mshikamano katika kushiriki ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Masjid Taqwa unaoendelea.

Na Mzidalfa Zaid

Hayo yamesemwa leo na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mohammedi Kadidi, wakati wa mkutano wa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa msikiti huo wa ghorofa tatu wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja, unaojengwa kwa nguvu za waumini wa dini hiyo.

Sauti ya shekhe Mkuu wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi

Akitoa taarifa ya awamu ya kwanza ya mradi huo, Katibu wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Jumaa Kifula, amesema mpaka sasa jumla ya shilingi milioni 249 tayari zimetumika katika hatua mbalimbali za ujenzi huo ambapo amewaomba wadau pamoja na waumini kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa msikiti huo ili kukamilisha mradi huo muhimu kwa jamii ya Kiislamu mkoani Manyara.

Picha ya Katibu wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Jumaa Kifula

Kwa upande wake, Katibu wa Vijana wa Kiislamu BAKWATA Mkoa wa Manyara, Abduri karim, pamoja na mmoja wa wadau wa maendeleo ya msikiti huo Aisha Kideso wamesema kuwa ujenzi wa Masjid Taqwa utasaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili katika jamii, hivyo wameitaka jamii kujitokeza kushiriki na kuunga mkono ujenzi huo.

Picha ya baadhi ya waumini