FM Manyara
FM Manyara
4 June 2026, 4:21 pm

Wanakikundi cha taarifa na maarifa kutoka kata ya Mamire Wilayani Babati Mkoani Manyara wamezipongeza wizara za Afya, Elimu na maji kwa kuweka kipaumbele mrengo wa jinsia kwenye bajeti zao ambazo zilishawasilishwa kwenye Bunge la 13 linaloendelea huko Jijini Dodoma.
Na Marino Kawishe
Akihitimisha majadiliano ya siku mbili ya wana KC Mamire, mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa Mkoani Manyara Clara Malley amesema bado Kuna baadhi ya wizara hazionyeshi moja kwa moja namna zitakavyoweka kipaumbele kwenye Bajeti ambazo vinamrengo wa kijinsia.
Aidha kwa upande wa baadhi ya wanakikundi waliozungumza na muandishi wa habari wamesema pongezi zao zinaenda moja kwa moja kwenye wizara zilizoonesha kuthamini kile wanachokipambania kwa muda mrefu kutokana na maazimio wanayoweka kwenye vikao vyao vinavyojadili masuala ya Jinsia.

