FM Manyara

So They Can Tanzania yawezesha wananchi kupata matibabu Babati

9 September 2025, 11:06 am

Picha ya wananchi wakisubiri kupatiwa huduma ya vipimo na matibabu

Na Marino Kawishe

Zaidi ya Wananchi elfu Tatu kutoka kata nne za Galapo, Mamire, Endakiso na Qash zilizopo Wilayani Babati Mkoani Manyara wamejitokeza kupata huduma za afya katika kambi ya siku tano iliyomalizika jumamosi sept 6 iliyoandaliwa na Shirika la So They Can Tanzania kwa ushirikiano na Hospital ya halmashauri ya wilaya Babati.

Akizungumzia mafanikio ya kambi hiyo Afisa Maendeleo kutoka Shirika la STC Bi Dorine Mwandangwa amesema kwenye zoezi hilo hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na wanaishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia Madaktari ambao wamejitolea kutoa huduma mbali mbali kwenye Kambi hiyo.

Sauti ya Afisa Maendeleo kutoka Shirika la STC

Kwa upande wake Mratibu wa Madaktari hao katika kambi hiyo Dr Silvia Nyange kutoka hospitali ya wilaya ya Babati pamoja Mwenyekiti wa Wazazi mahiri kutoka Kata ya Galapo Zakaria Geray na wamesema wagonjwa wengi waliojitokeza wanasumbuliwa na macho wakifwatiwa na magonjwa mengine na wamelishukuru Shirika hilo kwa kuguswa katika kutoa huduma za afya kwa wananchi ambao wengi wao hawana uwezo wa kumudu matibabu.

Kumalizika kwa Zoezi hilo ni maandalizi ya kambi nyingine ijayo ambayo itafanyika katika kata zote nne ambazo Shirika la STC wamekuwa wakitoa huduma za elimu na sasa wakijikita kutoa huduma za afya. 

Picha ya Dokta Silvya Nyange akimhudumia mgonjwa wa macho