FM Manyara
FM Manyara
1 July 2026, 12:54 am

Na Emmy Peter
Wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Manyara wamehimizwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati, na ubora unaotakiwa ili kuwanufaisha wananchi.
Maelekezo hayo yametolewa leo na mkuu wa wilaya ya Hanang Halmish Hazal aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga katika warsha ya wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoandaliwa na Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara.
Awali akizungumza katika warsha hiyo mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema lengo la warsha hiyo ni kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuzingatia uwajibikaji, matumizi sahihi ya rasilimali za umma na kuzuia vitendo vya rushwa vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wa miradi.