FM Manyara
FM Manyara
31 July 2026, 7:37 pm

Ikiwa Maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yanaanza kesho Agasti mosi jamii Wilayani Babati mkoani Manyara imehaswa kuzingatia umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto kwa kutambua umuhimu wa kumnyonyesha mtoto pindi anapozaliwa kwa wakati na ulio sahihi .
Na George Augustino
Hayo yamesemwa leo na Afisa lishe kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Laurencia Urio alipozungumza na Fm Manyara, amesema lengo la uanzishwaji ya wiki ya unyonyeshaji duniani ni kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto ili kuimarisha afya za watoto.
Kwa upande wake Muuguzi kutoka Hospitali ya Mji wa Babati Restituta amesema uimarishaji wa unyonyeshaji unaanzia wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ambapo mama anatakiwa kuwa na afya njema kwa kuzingatia kula vyakula vyote vyenye virutubisho muhimu ili maziwa yaweze kutoka kwa wingi.
Kauli mbiu ya wiki ya unyonyeshaji kitaifa ni “Mwanzo imara wa maisha ya Mtoto, huanza na maziwa ya Mama“