FM Manyara

TMA Manyara yatoa tahadhari mvua za elinino

15 September 2026, 8:53 am

Picha ya meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma amour 

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za mvua za elinino ambazo zimetabiriwa kunyesha hivi karibuni.

Na Mzidalfa Zaid

Mamalaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA) mkoa wa Manyara imeendelea kutoa tahadhari kwa wafugaji,wakulima, wavuvi na wananchi kwa ujumla kufuatia kuwepo kwa mvua za elinino zinazotarajiwa kuanzia wiki ya kwanza mwezi wa Kumi mwaka huu.

Wito huo umetolewa na meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma amour , amesema mvua hizo za elinino zitaleta madhara mbalimbali ikiwemo mafuriko na magonjwa hivyo Wananchi wanapaswa kuchukua hatua za haraka za tahadhari.

Sauti ya meneja wa TMA mkoa wa Manyara Salma amour

Kwa upande wake afisa mwangazi wa hali ya hewa mkoa wa Manyara Haji Hamimu amewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa za Kila siku ili kujua mwenendo wa hali ya hewa.

Sauti ya afisa mwangazi wa hali ya hewa mkoa wa Manyara Haji Hamimu