FM Manyara

NIDA Manyara kuadhimisha siku ya utambulisho

14 September 2026, 11:47 am

Picha ya Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Manyara Abubakari Kalinga akiwa katika studio za fm Manyara akizungumza katika kipindi(Picha na Hawa Rashid)

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA mkoa wa Manyara inatarajia kugawa vitambulisho vya nida siku ya utambulisho duniani katika viwanja vya stendi ya zamani ambapo kaimu mkuu wa wilaya ya Babati anatarajia kuwa mgeni rasmi.

Na Mzidalfa Zaid

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya utambulisho Duniani yanayotarajiwa kufanyika Septemba 16 mwaka huu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mkoa wa Manyara itatumia siku hiyo kuwafikishia wananchi vitambulisho vya Taifa ambavyo tayari vimesajiliwa na kukamilika.

Udzungwa Mountain National Park

Akizungumza na FM Manyara, Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Manyara, Abubakari Kalinga, amesema NIDA imeweka utaratibu wa kuwatumia wananchi ujumbe mfupi wa simu (SMS) pindi vitambulisho vyao vinapokuwa tayari, ili kuwawezesha kufika katika ofisi za NIDA na kuvichukua.

Sauti ya Afisa Msajili wa NIDA Mkoa wa Manyara, Abubakari Kalinga

Kalinga amesema utaratibu huo umesaidia kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho, huku wananchi wakitakiwa kuzingatia ujumbe wanaotumiwa na NIDA na kufika katika ofisi husika kwa ajili ya kuchukua vitambulisho vyao.

Aidha, amesema katika kipindi cha mwezi Septemba, NIDA Mkoa wa Manyara imeendelea kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mkoa.

kwa habari mbalimbali unaweza kutusikiliza kupitia link hii

https://radiotadio.co.tz/fmmanyara/