FM Manyara

RC Shigela akutana na viongozi wa kimila na kidini Manyara

17 September 2026, 6:55 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, leo amekutana na wazee wa kimila pamoja na viongozi wa dini

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, leo amekutana na wazee wa kimila pamoja na viongozi wa dini mkoani humo kwa lengo la kufanya mazungumzo, kusikiliza ushauri na kuomba baraka kwa ajili ya Mkoa wa Manyara.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shigela amesema viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo, amani na ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Manyara.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela
Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Peter Toima, amehudhuria mkutano huo na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo pamoja na mikakati ya kuendelea kuimarisha ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Manyara.

Kwa upande wao, wazee wa kimila wamepata fursa ya kueleza kero na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao, huku wakitoa maoni na ushauri kwa viongozi kuhusu namna bora ya kuzitatua.

Sauti ya wazee wa dini na viongozi wa kimila
Picha ya baadhi ya wazee na viongozi wa dini

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, wazee wa kimila na viongozi wa dini katika kuhakikisha Mkoa wa Manyara unaendelea kuwa na amani, mshikamano na maendeleo.

Picha ya baadhi ya viongozi wa dini na viongozi wa kimila