FM Manyara

Jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya lapata vitendea kazi

25 May 2026, 4:51 pm

Picha ya baadhi ya vitendea kazi ambavyo vimekabidhiwa kwa jeshi la zima moto na uokoaji wilaya ya Babati

Kaimu mkuu wa wilaya ya Babati ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Remidius Mwema , amewataka viongozi wa jeshi la zima moto na uokoaji wilayani Babati mkoani Manyara kutoa elimu kwa wananchi namna ya kukabiliana na majanga kwa kutumia vifaa vya kuzimia moto.

Na Mzidalfa Zaid

Mwema amesema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa jeshi la zima moto na uokoaji yakiwemo magari,mitambo na boti,  ambapo amesema wananchi wengi hawajui namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto ambapo amewataka viongozi hao wa jeshi la zima moto kutoa elimu kwa jamii namna ya kutumia vizimia moto.

Sauti ya Kaim mkuu wa wilaya ya Babati ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Remidius Mwema
Picha ya sauti ya Kaim mkuu wa wilaya ya Babati ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Remidius Mwema akikabidhi vifaa vya kuzimia moto kwa wananchi wa Babati.

Kwa upande wake mkuu  wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Babati Emmanuel Kibona amesema vitendea kazi hivyo vina thamani ya shilingi billioni 2.4 ambapo amesema vifaa hivyo vitasaidia kurahisisha kazi ya uokoaji  kwa wakati .

Sauti ya mkuu  wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya Babati Emmanuel Kibona