FM Manyara

Magari ya kusafirisha wanafunzi yakaguliwa Manyara

7 June 2026, 3:55 pm

Picha ya baadhi ya magari ya shule yakikaguliwa

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Manyara Michael Mwakasungula ameongoza zoezi la ukaguzi wa magari yanayosafirisha watoto katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa watoto wakati wa kipindi hiki cha likizo .

Na Emmy Peter

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwakasungula amesema lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha watoto wanaosafiri katika kipindi cha shule wanakuwa salama na kufika katika shule bila kupata madhara yanayoweza kuepukika kwa ubovu wa vyombo vya Moto.

Sauti ya Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Manyara

Kwa upande wao, baadhi ya madereva WA shule wameeleza kuwa ukaguzi huo ni muhimu kwani unasaidia kuongeza usalama na kuwakumbusha wajibu wao wa kulinda maisha ya watumiaji wa barabara na Watoto kwa ujumla.

Sauti ya baadhi ya madereva

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limeendelea kusisitiza ushirikiano wa wananchi na wadau wa usafiri ili kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua na usalama unaimarika katika kipindi chote cha likizo za shule.