FM Manyara
FM Manyara
25 May 2026, 5:08 pm

Mkoa wa Manyara unatarajia kufanya mbio za hisani za kuchangia uboreshaji wa huduma za watoto wachanga na watoto njiti zijulikanazo kama Manyara Tanzanite Marathon zenye kauli mbiu ya “hatua moja, okoa maisha ya mtoto” zinazotarajiwa kufanyika Agosti 22, 2026 katika mji wa Babati.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mbio hizo ambapo amesema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba
Mh. Sendiga amesema lengo la mbio hizo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kwa watoto wachanga katika mkoa wa Manyara pamoja na kujenga jengo la watoto wachanga katika hospitali ya wilaya ya Hanang.
Ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki na kuchangia katika mbio hizo kwa lengo la kuokoa maisha ya watoto wachanga na kuboresha sekta ya afya mkoani manyara.
Aidha , amesema ili kufanikisha ushiriki wako, unaweza kulipia mchango wako kwa kutumia Lipa Namba ya Vodacom (M-Pesa) ambayo ni 352193766, au kutumia Lipa Namba ya Yas ambayo ni 435296353, ambapo namba zote mbili zinasomeka kwa jina la usajili la MANYARA TANZANITE MARATHON.
