FM Manyara
FM Manyara
28 May 2026, 9:11 pm

Wakati Bunge la 13 likiendelea Jijini Dodoma na Wizara mbali mbali zikiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2026-2027 vituo vya taarifa na maarifa Mkoani Manyara vimepata wasaa wakujadili bajeti za Wizara ya Afya, Elimu, Maji na Kilimo ambazo zilishawasilisha bajeti zao.
Na mwandishi wetu
Akizungumza mbele ya Wanakikundi cha taarifa na maarifa cha Mamire Mratibu wa vikundi hivyo mkoani Manyara Clara Malley amesema lengo la Majadiliano hayo nikutoa maoni ya pamoja ambayo yatafanyiwa kazi na mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP kuona iwapo bajeti hizo zimelenga mrengo wa Jinsia.

Nao badhi ya wanakikundi cha taarifa na maarifa kutoka kata ya Mamire wamesema walifwatilia Bajeti hizo na kuona zinakidhi takwa lao japo Kuna baadhi ya wizara ikiwemo Wizara ya kilimo haijabainisha moja kwa moja kipaumbele kwenye kilimo cha asili ambacho kinatajwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania kama kilimo chenye Tina kwa vituo hivyo.
Vituo hivyo vya taarifa na maarifa kutoka mkoani Manyara vinajumuisha kituo cha Mamire kilichopo Kata ya Mamire Wilayani Babati na Murray kilichopo Kata ya Murray Wilayani Mbulu.
