FM Manyara
FM Manyara
17 August 2026, 10:36 pm

Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP umafanya mafunzo ya siku mbili kwa baadhi ya Viongozi kutoka serikali ngazi ya vijiji na kata na wadau mbali mbali wanaojishughulisha na kutoa msaada kwa wahanga au manusura wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Na Marini Kawishe
Akizungumza na Fm Manyara Mwezeshaji kwenye mafunzo hayo Marcela Lungu amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuimarisha uwezo wa jamii katika kuzuia, kutambua, kuripoti, kutoa taarifa na kukabiliana na ukatili wa kijinsia ambao kwa kiwango kikubwa upo kwenye jamii.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza leo Agust 17 na kumalizika kesho agust 18 wamesema kupatiwa mafunzo kama hayo yamewaongezea uelewa wakukabiliana na ukatili wa kijinsia ambao unafanyika kwenye jamii na mazingira tofauti na jamii nyingi
Mafunzo hayo yanatarajia kuweka mkakati wa pamoja ili kuondoa vikwazo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na uwajibikaji katika mnyororo wa huduma za ukatili kwa kuandaa mpango kazi wenye kubainisha majukumu na wajibu wa wahusika wenye ushawishi katika jamii pamoja na serikali.
