FM Manyara

Kaimu DC Babati aonya upotoshaji kampeni ya chanjo ya polio

26 August 2026, 6:46 pm

Picha ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema akiwa katika kikao cha mafunzo ya kampeni ya chanjo ya polio kwa Viongozi na wadau wengine wa Halmashauri ya Mji wa Babati.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema amewataka Viongozi wote waliohudhuria mafunzo ya Chanjo ya Polio itakayoanza kutolewa kesho alhamis August 27 hadi 30 mwaka huu 2026 kwenye halmashauri ya wilaya ya Babati kuzingatia elimu waliyopatiwa na kuacha kupotosha taarifa za kampeni hiyo ya chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka kumi.

Na Marino Kawishe

Akizungumza kwenye kikao kazi cha wadau mbali mbali kutoka kwenye jamii wakati wawasilisho la kampeni ya Chanjo ya Polio amesema Kuna baadhi ya maeneo unakuta kiongozi wa eneo husika hajaelewa kinachofanywa huku akisisitiza Viongozi wanapoelewa jambo lolote linalofanywa na Serikali basi na wananchi inakuwa rahisi kuelewa.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati Remidius Mwema

Zoezi la chanjo ya polio kitaifa litazinduliwa Wilayani Kiteto mkoani Manyara hapo kesho August 27 na mpango huu wa kampeni ya chanjo ya polio kitaifa  utahusisha mikoa nane ambayo ni Manyara, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam  na Mara.