FM Manyara
FM Manyara
1 October 2026, 5:37 pm

Leo ikiwa ni siku ya wazee duniani , wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuwathamini wazee na kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo huduma za afya, malazi na chakula.
Na Mzidalfa Zaid
Jamii mkoani Manyara imetakiwa kuwathamini wazee kwa kuwaepusha na vitendo vya ukatili pamoja na kuwa haki zao stahiki.
Hayo yameelewa leo na mwenyekiti wa wazee mkoa wa Manyara Jasson Idei wakati akiongea na fm Manyara, amesema kila mwananchi ana wajibu wa kuwalinda wazee.
Aidha, amesema wazee wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya ukatili ambapo amekemea vitendo hivyo ambvyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya wananchi.