FM Manyara

Mvua za elinino hazitanyesha Manyara-Chief Dodo

9 October 2026, 1:57 pm

Picha ya Chief wa kabila la wagoroa chief dodo

Kufuatia kutabiriwa mvua za elinino hapa nchini , Chief wa kabila la wagoroa chief Dodo amesema wamefanya maombi ya kutonyesha mvua za elinino katika mkoa wa Manyara.

Na Mzidalfa Zaid

Chief wa kabila la wagoroa chief Dodo ,amesema wamefanya maombi ya kuzuia mvua za elinino ambapo amewataka wananchi waendelea kumuomba Mungu kuepusha janga hilo

Akiongea na Fm Manyara chief dodo amesema kwa Imani wlaiyonayo mvua za elinino hazitanyesha katika mkoa wa Manyara, badala yake zitanyesha mvua za kawaida.

Sauti ya Chief wa kabila la wagoroa chief Dodo

Baadhi ya wananachi mkoani Manyara wamesema wameshachukua tahadhari za kujikinga na mvua hizo huku wakiiomba serikali kuboresha maeneo yanayopitisha maji.

Sauti ya wananchi