FM Manyara
FM Manyara
9 November 2026, 4:27 pm

Mradi wa nishati Jadidifu wa Kakute wawanufaisha wanufaika 320 kupitia mradi unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati katika jamii
Na Diana Juma
Taasisi ya Kakute Projects imewafikia wanufaika 320 katika wilaya za Babati na Monduli mkoani Manyara pamoja na Arusha, kupitia mradi wa nishati jadidifu unaolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati katika jamii ambazo hazijafikiwa kikamilifu na huduma za umeme.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Afisa mradi wa Restore kutoka Kakute Projects, Jumanne Sasita, amesema Taasisi hiyo inatumia teknolojia mbalimbali zikiwemo majiko banifu, mifumo ya nishati ya jua pamoja na pampu za maji zinazotumia nishati ya jua ili kurahisisha shughuli za wananchi.
Aidha, Sasita amesema miongoni mwa mafanikio ya mradi huo ni kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma kupitia mafunzo ya ufundi wa mifumo ya nishati ya jua pamoja na kuwapatia ujuzi wa kutengeneza majiko banifu.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha vijana kujiajiri na kutumia ujuzi walioupata kutoa huduma katika jamii zao, na ikichochea matumizi ya nishati safi na endelevu.
