FM Manyara

Ulega awaagiza watendaji Manyara kushughulikia malalamiko ya wananchi

26 October 2026, 6:37 pm

Picha ya waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega

Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, amewataka watendaji wote mkoani Manyara kuhakikisha wanashughulikia malalamiko yanayotolewa na wananchi na kutoa mrejesho kwa wakati, huku malalamiko yaliyo nje ya mamlaka yao yafikishwe kwa mamlaka husika kwa hatua zaidi.

Na Mzidalfa Zaid

Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega amewataka Viongozi mkoani Manyara kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao kwa wakati.

Ulega ameyasema hayo leo oktoba 26 ,2026 mkoani Manyara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu ya uraia na utawala bora kwa viongozi na watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa, ambapo amesisitiza umuhimu wa watendaji kuwa wawazi kwa wananchi wanaowahudumia.

Sauti ya Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega

Aidha, amewataka viongozi kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, wazee na watu wenye mahitaji maalumu, huku akisisitiza kuwa katika kushughulikia migogoro, ni muhimu kusikiliza pande zote zinazohusika ili kupata suluhu ya haki na kuzuia malalamiko kujirudia.

Picha ya Waziri wa Katiba na Sheria Abdallah Ulega akizungumza na watendaji mkoani Manyara

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt Seif Shekalaghe amesema mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uelewa wa Katiba, sheria, elimu ya uraia na utawala bora ambapo amesema hadi sasa, jumla ya watendaji 5,111 katika mikoa 17 wamepatiwa mafunzo hayo katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt Seif Shekalaghe
Picha ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt Seif Shekalaghe

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amesema mafunzo hayo yatasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi mkoani hupa, ikiwemo migogoro ya ardhi inayochangiwa na ukiukwaji wa sheria.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela,
Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela

Mafunzo hayo yaliyoanza leo mkoani Manyara yanatarajiwa kutolewa katika halmashauri zote za mkoa wa Manyara, yakihusisha watendaji kuanzia ngazi ya vijiji na kata hadi halmashauri.

Picha ya baadhi ya washiriki