FM Manyara
FM Manyara
18 October 2026, 3:43 pm

Wananchi mkoani Manyara wameshauriwa kutembelea na kujionea maonesho ya wanyamapori mbalimbali yanayoendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, Babati, ikiwa ni sehemu ya maonesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2026.
Na Mzidalfa Zaid
Katika maonesho hayo Kuna wanyama mbalimbali wakiwemo simba, fisi, chatu, mamba na nungu mrusha mishale, yakilenga kuwapa wananchi fursa ya kuwaona wanyama hao na kujifunza kuhusu wanyamapori.

Akizungumza kuhusu maonesho hayo mwakilishi wa kampuni hiyo abas Abdul amesema gharama za kiingilio ni nafuu, ambapo mtu mzima anatakiwa kulipa shilingi 3,000 huku watoto wakilipia shilingi 2,000 ili kujionea wanyama hao.