FM Manyara

Wananchi Manyara wahimizwa kutumia Takwimu za NBS

17 October 2026, 10:54 pm

Picha ya Meneja wa Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Manyara, Gidion Mokiwa,

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kutumia takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuboresha utendaji wa shughuli za kiuchumi na kupanga mipango ya maendeleo.

Na Mzidalfa Zaid

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imewataka wananchi kutumia takwimu rasmi zinazottolewa na ofisi hiyo ili kisaidia katika mipango mikakati mbalimbali.

Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Manyara, Gidion Mokiwa, wakati wa Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea mkoani humo.

Sauti ya Meneja wa Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Manyara, Gidion Mokiwa

Mokiwa amesema matumizi sahihi ya takwimu ni muhimu katika kufanya maamuzi yenye tija, kuongeza ufanisi katika shughuli za kiuchumi na kuwezesha wananchi kupanga mipango yao ya maendeleo kwa kuzingatia taarifa sahihi.