FM Manyara

Wakulima Mamire watakiwa kuanzisha ushirika kulinda mbegu za asili

27 November 2026, 5:48 pm

Picha ya baadhi ya wakulima

Wakulima wa kata ya Mamire Wilayani Babati Mkoani Manyara wametakiwa kuanzisha ushirika wakutambua na kuhifadhi mbegu za asili ili kulinda mazao hayo na kuepukana na utapeli ambao unaweza kufanywa na watu kutoka mbali na eneo hilo.

Na Marini Kawishe

Akizungumza na wakulima wa  kikundi cha taarifa na maarifa kilichopo katika kata hiyo kwenye warsha ya siku mbili  chini ya Mtandao wa jinsia Tanzania ( TGNP) Mwezeshaji wa  jukwaa la jinsia Tanzania  Rebecca Mjema amesema inapaswa wakulima kufanya usajili wa ushirika wao nakutambuliwa kisheria ili kulinda haki za wakulima  wa mbegu za asili.

Sauti ya Mwezeshaji wa  jukwaa la jinsia Tanzania  Rebecca Mjema

Nao baadhi ya washiriki  kwenye semina hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi yaletayo athari kwa wanawake na wanaume  akiwemo mratibu wa Vikundi hivyo mkoani Manyara Clara Malley pamoja na Mkt wa kc ya Mamire  Magreth Baso wamesema kwa sasa wanazalisha mbegu za asili ikiwemo mahindi na mbegu nyingine ila bado hawajatambulika rasmi nakupata usajili ambo utaweza kulinda mbegu  zao kisheria. 

Sauti ya washiriki

Warsha hiyo ya siku mbili imewakutanisha wanachama wa kituo cha taarifa na maarifa kutoka kata ya Mamire ambao walipata wasaa wakueleza kiunagaubaga changamoto mbali mbali zinazotokea wakati wa mabadiliko ya Tabia Nchi kwenye jamii wanakotoka.

Picha ya baadhi ya washiriki