FM Manyara

Milioni 109 za posho hewa Burunge WMA zarejeshwa

3 November 2026, 10:03 pm

Picha ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Anthony Gang’olo

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara imefanikisha kurejesha kiasi cha Shilingi Milioni 109 ambazo zilikuwa zimetafunwa na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (Burunge WMA).

Na Mzidalfa Zaid

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Anthony Gang’olo amesema fedha hizo zilichukuliwa kwa njia ya malipo ya posho hewa na posho za kila mwezi zisizo na uhalali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025.

Sauti ya Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Anthony Gang’olo

Gang’olo amesema kuwa baada ya operesheni maalum iliyofanywa na taasisi hiyo, fedha zote zimerejeshwa katika akaunti ya Jumuiya hiyo inayojumuisha vijiji 10.

Aidha , TAKUKURU imeagiza Katiba ya Jumuiya ya Burunge WMA ifanyiwe marekebisho ili kuziba mianya yote iliyokuwa ikitumika kufanya ubadhirifu ambapo TAKUKURU imetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia namba ya bure 113.