FM Manyara

Wafanyabiashara wahimizwa kushiriki maonesho ya Tanzanite Manyara trade fair

13 October 2026, 9:25 am

Picha ya Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) Mkoa wa Manyara Lerunde Laizer

Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanaendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara, huku wafanyabiashara na wadau mbalimbali wakihimizwa kushiriki katika maonyesho hayo ili kutangaza na kukuza biashara zao.

Na Mzidalfa Zaid

Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) Mkoa wa Manyara Lerunde Laizer, amesema maonyesho Tanzanite Manyara trade fair yanatarajiwa kuanza Oktoba 15 na kumalizika Oktoba 21 mwaka huu .

Amesema maonyesho hayo yatatoa fursa kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali kuonyesha bidhaa na huduma zao, kutangaza biashara zao pamoja na kupanua wigo wa masoko na kupata fursa mpya za kibiashara.

Sauti ya Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) Mkoa wa Manyara Lerunde Laizer

Aidha, Laizer amewataka wafanyabiashara, wajasiriamali na wadau wengine kutumia fursa hiyo kushiriki kikamilifu katika maonyesho hayo kwa lengo la kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi.