FM Manyara

Serikali yaahidi kuongeza visima vya maji Hanang

7 October 2026, 9:44 pm

Picha ya naibu waziri wa maji Kundo Mathew

Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Hanang’ kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.

Na Mzidalfa Zaid

Naibu waziri wa Maji Kundo Mathew ameelekeza mamlaka za maji mkoani Manyara kuhakikisha ifikapo 2030 Kila kijiji katika wilaya ya Hanang kinafikiwa huduma ya maji.

Kundo amesema hayo leo wilayani Hanang’, mkoani Manyara, wakati akiendelea na ziara yake mkoani humo, ambapo amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara kuhakikisha wananchi hawatembei zaidi ya kilomita mbili kufuata huduma ya maji, kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu na makazi yao. 

Sauti ya naibu waziri wa maji Kundo Mathew
Picha ya Naibu waziri wa maji Kundo Mathew akitoa maelekezo
Picha ya Naibu waziri wa maji

Awali, Mbunge wa Jimbo la Hanang’, Asia Halamgha, amemuomba Naibu Waziri wa Maji kuhakikisha fedha zinapelekwa wilayani humo kwa ajili ya kuchimba visima katika maeneo ambayo hayana huduma ya maji, ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Hanang’, Asia Halamgha,

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang’… amesema maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Maji yatatekelezwa kwa wakati, huku akisisitiza ushirikiano wa wananchi katika kulinda na kutunza miundombinu ya maji.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Hanang wameishukuru serikali kwa kuwaletea huduma ya maji katika maeneo yao kwani kwa muda mrefu walikuwa wakimfuata huduma ya maji kwa kutembea Zaidi ya kilomita 5 kufuata maji.

Picha ya baadhi ya wananachi wakiwa na naibu waziri wa maji