FM Manyara
FM Manyara
26 November 2026, 5:57 pm

Shirika la STC Tanzania limeungana na serikali katika maadhimisho ya siku 16 zakupinga ukatili kwa watoto na wanawake ambazo zimezinduliwa rasmi hapo Jana November 25 na zitakazomalizika Dec 10 mwaka huu 2026.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na Fm Manyara Radio Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo nchini Tanzania Roselyne Mariki amesema kila mmoja anao wajibu wakutoa taarifa ya matukio ya ukatili yanaofanywa kwenye jamii na kuendelea kushirikiana na serikali ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wazazi mahiri wanaofanya kazi kwenye Kanda ya Galapo yenye muunganiko wa kata za Galapo, Qash Endakiso na Mamire Zakaria Deray amesema wanaendelea kutoa elimu yakupinga aina zote za ukatili na hali ya ukatili kwenye eneo hilo inapungua siku hadi siku.
Siku 16 zakupinga ukatili kwa wanawake na watoto huadhimishwa kila mwaka kwa lengo lakufikisha elimu kwa jamii na kuripoti matukio ya ukatili pamoja nakuwatambua wahanga wa ukatili waliopo kwenye jamii.