FM Manyara
FM Manyara
9 November 2026, 9:56 am

Shekhe wa Mkoa wa Manyara, Mohamed Kadidi, ameitaka jamii kujiepusha na vitendo vya rushwa akieleza kuwa vitendo hivyo vina madhara makubwa katika jamii, ikiwemo kudhoofisha haki, uadilifu na uwajibikaji.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuacha kuomba au kupokea rushwa kwani rushwa imekatazwa na Mwenyezi Mungu .
Akizungumza na FM Manyara, Shekhe Kadidi amesema rushwa ni miongoni mwa vitendo vinavyokwamisha maendeleo ya jamii na kusababisha baadhi ya watu kukosa haki zao, hivyo amewataka wananchi kuzingatia misingi ya maadili mema na kujiepusha na vitendo hivyo.
Aidha, amewataka wazazi na walezi mkoani Manyara kuwalea watoto wao katika misingi ya dini kwa kuwapatia elimu ya kiroho tangu wakiwa wadogo, akieleza kuwa mtoto anayejengewa hofu ya Mungu huwa na uwezekano mkubwa wa kutenda matendo mema na kujiepusha na vitendo viovu.
