FM Manyara
FM Manyara
8 August 2025, 12:26 pm

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara Faki Lulandala, amewataka wakulima, wavuvi na wafugaji kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na halmashauri kukuza mitaji Yao na kujiinua kiuchumi.
Na Mzidalfa Zaid
Lulandala ametoa wito huo mkoani Arusha ,alipokuwa mgeni rasmi wa zamu katika maonesho ya wakulima kanda ya kaskazini yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, amesema serikali ya awamu ya sita imetoa fursa ya kutoa mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri zote nchini,hivyo vijana wanaotaka mikopo hiyo wajiunge kwenye vikundi na wanufaike na mikopo hiyo, huku akisema amefurahishwa na ubunifu ambao umefanywa na washiriki wa maonesho hayo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu, amesema halmashauri yake imeshiriki maonesho hayo kwa kutoe elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kisasa.

Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo, wamesema maonesho ya mwaka huu yamekuwa makubwa kwa kuwa wananchi wengi wanatembelea mabanda kujionea bidhaa zinazopatikana katika maonesho hayo huku wakielezea namna wanavyoyatumia maonesho hayo kutangaza biashara zao.