FM Manyara

Parokia mpya ya Mrara Jimbo Katoliki la Mbulu yazinduliwa

17 April 2026, 12:25 am

Picha ya Maaskofu wa majimbo katoliki ya Mbulu,Geita na Bunda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Babati Emanuela Kaganda

Na George Augustino.

Mkuu wa wilaya ya Babati Mkoani Manyara EmanuelaKkaganda amewaomba viongozi wa dini kuendelea  kuzuia mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa mafundisho ya imani  pamoja na kuiombea amani nchi ya tanzania ili amani na utulivu uzidi kutawala.

Dc Kaganda ameyasema hayo leo katika sherehe ya uzinduzi wa Parokia mpya Mtakatifu Anna  ya Mrara ya Jimbo Katoliki la Mbulu, sherehe iliyohudhuriwa na Askofu mwenyeji wa Jimbo Katoliki la Mbulu Mhashamu Baba Askofu Anton Lagwen, Askofu wa jimbo katoliki  la Geita Flavian Kasala, Askofu wa Jimbo Katoliki la  Bunda Simon Masundora, Mapadre mbalimbali pamoja na waumini wa Parokia mbalimbali ikiwemo Parokia mpya ya Mrara.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Babati

Kwa upande wake Muasham Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anton Lagwen amezindua  na kuitangaza  rasmi parokia ya mrara kuwa parokia kamili pamoja na  kumtangaza Padre  Yuda Aley  kuwa Paroko wa kwanza wa Parokia hiyo mpya ya Mrara.

Sauti ya Muasham Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu
Picha ya Muasham Baba Askofu Anton Lagwen akimkabidhi nyaraka mbalimbali za Parokia mpya ya Mrara Paroko wa Parokia hiyo Yuda Aley

Mwaka 2023 Muasham Baba Askofu Anton Lagwen alikipandisha hadhi kigango cha Mrara na kuwa Parokia ndogo na mwaka 2024 akaipandisha hadhi Parokia ndogo ya Mrara na kuwa Parokia teule ya mrara yenye Jumuiya ndogo ndogo 10  na jumla ya waumini 1,261 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2025 na hatimaye leo kutangazwa kuwa parokia kamili ya Mrara.

Picha ya Watoto wa Parokia ya Mrara wakipata Sakramenti ya Kipaimara