FM Manyara

Madereva Manyara wahimizwa kusajili stika za kidigitali

23 July 2026, 4:49 pm

picha ya Sajenti Said Yussuf kutoka Ofisi ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara(kushoto) na picha ya mtoa elimu kutoka Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Dotto Aloyce(kulia)

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara limetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya stika ya wiki ya “Nenda kwa Usalama Barabarani” kwa njia ya kidijitali.

Na Mzidalfa Zaid

Elimu hiyo imetolewa na Sajenti Said Yussuf kutoka Ofisi ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, ambaye amesema kuwa ili kujisajili kwa ajili ya kupata stika hiyo, mwombaji anatakiwa kuwa na simu janja (smartphone) itakayomwezesha kufanya usajili kwa njia ya mtandao.

Sauti ya Sajenti Said Yussuf kutoka Ofisi ya Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara,

Kwa upande wake, mtoa elimu kutoka Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Dotto Aloyce, amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanapeleka vyombo vyao kukaguliwa mara kwa mara ili kubaini hitilafu zinazoweza kujitokeza na kuzifanyia marekebisho mapema, hatua ambayo itasaidia kuongeza usalama wao wanapotumia barabara.

Sauti ya mtoa elimu kutoka Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Dotto Aloyce,