FM Manyara

Pelum Tanzania yawataka wakulima kutumia mbegu za asili

6 June 2025, 5:34 pm

picha ya mbegu za asili

Wakulima mkoani Manyara wametakiwa Kutumia mbegu za asili kwenye kilimo ili kupata faida na kunufaika na mazao yake.

Na Marino Kawishe

Shirika lisilo la kiserikali la Pelum Tanzania  limewataka wakulima wilayani Babati mkoani Manyara kuendeleza kilimo cha mbegu za asili ambacho kimekuwa na tija kwa baadhi ya maeneo hapa nchini. 

Akizungumza na wakulima wadogo wa vijiji vya Endagile, Mwinkantsi, Kwaraa na Mamire katika  maonesho ya mbegu za asili,  afisa miradi na masuala ya jinsia  kutoka shirika hilo Anna Marwa amesema lengo lao nikuona wakulima hao wakinufaika zaidi na kilimo cha asili. 

sauti ya afisa miradi na masuala ya jinsia  kutoka shirika hilo Anna Marwa

Kwa upande wake afisa miradi kutoka COSITA mkoani Manyara  Agustino  Baloh  amewaasa wakulima kutumia elimu ya kilimo asili kwa kushirikisha wanafunzi wanaosoma kwenye shule za msingi ili wapate uelewa wa kilimo hicho.

sauti ya afisa miradi kutoka COSITA mkoani Manyara  Agustino  Baloh 

Aidha wakulima wa kilimo cha mbegu za asili wamelishukuru shirika la PELUM TANZANIA  na COSITA kwa elimu waliyotoa kwenye maeneo yao ambayo imewawezesha kuendeleza kilimo cha asili ambacho kimekuwa na faida kwao.

sauti ya wakulima
picha ya afisa miradi na masuala ya jinsia  kutoka shirika la PELUM TANZANIA  Anna Marwa , akitoa elimu kwa wakulima na wanafunzi