FM Manyara

DAS Babati awahimiza wananchi kushiriki mbio za hisani za Manyara Tanzanite Marathon

15 August 2026, 10:03 am

Picha ya baadhi ya washiriki wa mazoezi ya pamoja ikiwa ni hamasa kuelekea Manyara Tanzanite Marathon

Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati, Thobias Abwaro, ameongoza mazoezi ya pamoja leo, tarehe 15 Agosti 2026, ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea mbio za hisani za Manyara Tanzanite Marathon zitakazofanyika Jumamosi, tarehe 22 Agosti 2026.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Abwaro amewataka wananchi kuendelea kujisajili na kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo za hisani, ambazo zinalenga kuchangia katika kuokoa maisha ya watoto, hususan watoto wachanga na watoto njiti.

sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati, Thobias Abwaro

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Emmanuel Khambay, ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Manyara Tanzanite Marathon, akisema kufanya hivyo ni kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, katika juhudi za kuhakikisha maisha ya watoto wachanga na watoto njiti yanaokolewa.

sauti ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Emmanuel Khambay

Baadhi ya washiriki wa mazoezi hayo wamesema wamejitokeza kwa ajili ya kutoa hamasa kuelekea Manyara Tanzanite Marathon, huku wakiahidi kushiriki kwa wingi katika mbio hizo zitakazofanyika tarehe 22 Agosti 2026.

sauti ya washiriki
picha ya baadhi ya washiriki