FM Manyara
FM Manyara
17 September 2026, 11:36 am

Shirika la So They Can Tanzania (STC) linaendelea na Kambi ya matibabu ya siku sita katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Babati.
Na Marino kawishe
Wananchi wa Kata za Qash, Endakiso na Mamire wilayani Babati, mkoani Manyara, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kambi ya matibabu inayoendelea, huku zikisalia siku tatu kabla ya kambi hiyo kumalizika.
Akizungumzia tathmini ya siku tatu za awali za kambi hiyo inayoratibiwa na Shirika la So They Can Tanzania (STC), Afisa Habari wa shirika hilo, John Mwakipesile, amewashukuru wananchi waliojitokeza kupata huduma, akieleza kuwa huduma zote zilizotangazwa zimetolewa kikamilifu na madaktari waliopo katika kambi hiyo.

Aidha, baadhi ya wanufaika wa kambi hiyo kutoka Kijiji cha Orngadida, Kata ya Qash, wameishukuru STC pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Babati kwa kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi, huku wakiwataka wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma hizo kujitokeza na kupata matibabu.
Kambi hiyo ya afya ya siku sita inatarajiwa kufikia ukingoni Septemba 19, 2026, na hadi sasa imeshawafikia wananchi zaidi ya 750.
