FM Manyara
FM Manyara
21 April 2026, 6:40 pm

Taasisi ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma imeendesha mafunzo kwa waalimu walezi wa club za maadili, yenye lengo la kuzifahamu sheria ya maadili, katika sekta ya umma pamoja na muongozo wakufungua klabu za maadili katika shule za msingi hadi vyuo vikuu vilivyopo mkoani Manyara.
Na Marino Kawishe
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaj ameitaka kada ya waalimu kuendelea kwa moyo mmoja kufundisha maadili kwa wanafunzi kwakua wazazi wamekuwa wakijishughulisha na shughuli za utafutaji kutafuta fedha na kujisahau kwenye malezi.

Aidha kwa upande wake katibu msaidiz sekretarieti ya maadili ya umma kanda ya kaskazini Gerald Mwaitebele amesema lengo la mafunzo hayo kwa waalimu hao ni kuwajengea zaidi uwezo waalimu ambao ndio wanafundisha watoto kutoka ngazi ya chini ili baadae vijana hao wanapoingia katika mitaa wawe na maadili mema.
Nae Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Manyara Mugisha Garibona amekiri kupokea maelekezo ya Katibu tawala mkoa wa Manyara aliyeagiza mkoa mzima kuwepo na Klabu za wanafunzi zinazofundisha Maadili ya Viongozi wa umma.
Semina hiyo imewaleta pamoja waalimu wa shule mbali mbali za msingi na sekondari ambazo tayari zimeanzisha vilabu katika shule zao zinazofundisha maadili ya Viongozi wa umma kutoka Halmashauri tano za mkoa wa Manyara.
